HAZARD AWATAJA ANAOTAMANI KUCHEZA NAO CHELSEA - Darajani 1905

HAZARD AWATAJA ANAOTAMANI KUCHEZA NAO CHELSEA

Share This
Nyota wa Chelsea, Eden Hazard amekuwa akihusishwa kutakiwa na baadhi ya vilabu barani Ulaya, lakini haswa klabu inayotajwa kumuwania ikiwa ni klabu kutoka nchini Hispania, Real Madrid ambao wao wamekuwa wakimsaka nyota huyo toka dirisha la usajili la msimu uliopita. Nyota huyo raia wa Ubelgiji amefanyiwa mahojiano na kuulizwa anadhani ni wachezaji gani anatamani amgepata fursa kucheza nao Chelsea.

Nyota huyo mwenye miaka 27 kwa sasa aliwataja nyota wenzake wanaocheza timu ya taifa ya Ubelgiji ambao ni Kevin De Bruyne ambaye anaichezea klabu ya Mama site (Man city) pamoja na nyota mwengine kutoka klabu ya As Roma, Radja Nainggolan ambaye Chelsea imekuwa ikimfukuzia bila mafanikio.

Nyota huyo ataiongoza timu yake ya taifa ya Ubelgiji kwenye michuano ya kombe la dunia huko nchini Urusi ambayo yataanza mwezi Juni.

"Ubelgiji tuna timu nzuri, yenye wachezaji bora. Sio kwamba mimi ni mchezaji wa Chelsea ndio niache kuwataja wanaocheza Tottenham au klabu nyengine, hapana tupo pamoja" alisema nyota huyo alipohojiwa na chombo cha habari cha COPA90.

Kevin De Bruyne aliwai kucheza Chelsea bila mafanikio na baadae kuuzwa kwenda kwenye klabu ya Wolfburg na kwa sasa anaichezea klabu ya Man city ambayo amekuwa akifanya nayo vizuri.

No comments:

Post a Comment