GWIJI WA ARSENAL AWATAJA WACHEZAJI SITA WA CHELSEA - Darajani 1905

GWIJI WA ARSENAL AWATAJA WACHEZAJI SITA WA CHELSEA

Share This
Nyota wa zamani wa Chelsea, Romelu Lukaku ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Manyumbu (Man utd) ya jijini Manchester alishauri kuundwe mchezo maalumu ambao utajumuisha wachezaji nyota kutoka pande mbili yaani kusini na kaskazini ambapo alitoa ushauri huo akitaka kuleta kama mfumo uliokuwa ukitumika katika ligi ya mchezo wa kikapu ya nchini Marekani ambapo nyota wa timu za vilabu wa pande mbili za mashariki na magharibi hutengeneza vikosi vya timu mbili kisha kumenyana katika mchezo maalumu. Ndipo Lukaku nae akashauri kitu hicho kifanyike na kwenye soka pia haswa kwenye ligi kuu Uingereza.

Mara baada ya kutolewa kwa ushauri huo, nyota wa zamani wa klabu ya Arsenyani (Arsenal), Ian Wright ambaye kwa sasa anafanya kazi ya uchambuzi wa soka aliambiwa ataje kikosi ambacho anadhani kinafaa kuunda timu ya wachezaji 11 wa timu ya Kusini (Southern XI) ndipo nyota huyo akawataja wachezaji sita katika kikosi hicho cha wachezaji 11 huku akimtaja mchezaji mmoja tu kutoka kwenye klabu yake ya zamani huku kwa klabu ya Tottenham akiwataja wachezaji watatu.

Wachezaji wa Chelsea waliotajwa kwenye kikosi hicho, ni mlinda mlango, Thibaut Courtois, Cesar Azpilicueta, Marcos Alonso, N'golo Kante, Eden Hazard na Willian Borges.

Kikosi kamili ni hiki;

No comments:

Post a Comment