MCHEZO WA CHELSEA WAGHAIRISHWA - Darajani 1905

MCHEZO WA CHELSEA WAGHAIRISHWA

Share This
Chelsea itacheza mchezo wake wa marudiano katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya dhidi ya Barcelona siku ya tarehe 14-Marchi huko nchini Hispania, ambapo mchezo wa kwanza uliocheza Uingereza uliisha kwa sare ya 1-1, ambao ndio ulikuwa mchezo wa kwanza wa michuano hiyo kwa klabu hizo mbili katika hatua ya 16 bora. Lakini pia tarehe 18-Marchi, Chelsea itasafiri tena mpaka kwenye uwanja wa King Power kucheza dhidi ya Leicester city katika mchezo wa kombe la FA katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo. Hii inamaanisha nini?

Kutokana na michezo hiyo kuwa karibu na kupishana kwa siku nne, inamaanisha mchezo wa Burnley dhidi ya Chelsea ambao ulikuwa umepangwa kufanyika tarehe 17-Marchi utakuwa hauna nafasi na hivyo kughairishwa. Kutokana na ratiba ya mwanzo iliyotolewa ingemaanisha kuwa Chelsea ingecheza dhidi ya Barcelona tarehe 14, kisha tarehe 17 kucheza dhidi ya Burnley na kesho yake kucheza dhidi ya Leicester kwenye kombe la FA ambapo kiasili haiwezekani michezo miwili ndani ya siku mbili na hivyo kumaanisha mchezo wa ligi kuu dhidi ya Burnley kughairishwa.

No comments:

Post a Comment