SABABU YA AMPADU KUWA NJE - Darajani 1905

SABABU YA AMPADU KUWA NJE

Share This
Kwenye mchezo wa jana ambao Chelsea Youth ilicheza dhidi ya Fulham U18, ambayo ni timu chini ya miaka 18 kwenye michuano ya kombe la FA kwa hatua ya robo fainali na kuishuhudia Chelsea Youth kuondoka na ushindi ikiwa ugenini wa magoli 0-6, kuna wengi walishangazwa mara baada ya kukosekana kwa nyota Ethan Ampadu kwenye mchezo huo.

Nami kama nilivyokuahidi kuwa nitakuletea makala fupi ya kukuelezea sababu ya kwanini nyota huyo mwenye miaka 17 kukosekana kwenye mchezo huo.

Wiki iliyopita katika michuano ya klabu ya mabingwa Ulaya chini ya miaka 18, nyota huyo alijumuika na timu hiyo na kuisaidia kupata ushindi mnono wa mabao 5-2 dhidi ya Feyenoord, lakini nyota huyo raia wa Wales hakucheza mchezo wote kutokana na kupata majeraha na kumfanya kutolewa na hivyo kumfanya akose mchezo huo wa jana kutokana na kuwa na majeruhi.

Lakini inaaminika nyota huyo atakuwa sawa na kupona kabisa pale Chelsea Youth itakaposafiri na kwenda kucheza dhidi ya Real Madrid katika hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa Ulaya ambapo mchezo huo utachezwa tarehe 14.
Kikosi kamili kilichocheza kwenye mchezo huo wa jana kwenye uwanja wa Craven Cottage

No comments:

Post a Comment