CHELSEA YOUTH YAFIKA NUSU FAINALI KWA REKODI - Darajani 1905

CHELSEA YOUTH YAFIKA NUSU FAINALI KWA REKODI

Share This
Klabu ya vijana ya Chelsea Youth ambao ni chini ya miaka 18 wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la FA mara baada ya kuibamiza klabu ya Fulham ya chini ya miaka 18 maarufu kama Fulham U18 kwa magoli 0-6 ambapo Chelsea Youth walikuwa ugenini na kufanikiwa kupata ushindi huo mnono.

Ushindi huo ambao unawafanya Chelsea Youth kucheza nusu fainali ya tisa mfululizo ulipatikana mara baada ya kutoshana nguvu kipindi cha kwanza kwa kutoka sare ya 0-0 kwenye uwanja wa Fulham, Craven Cottage. Magoli ya Chelsea yalianza kufungwa mnamo dakika ya 51 kwa goli la kujifunga ambapo mchezaji wa Fulham, Mundle-Smith ndiye alijifunga akijitahidi kuokoashuti lililopigwa na nyota wa klabu ya Chelsea, Hudson-Odoi, lakini hiyo haikuwa sababu ya kumfanya nyota huyo ashindwe kufunga goli jengine mara baada ya dakika tano baadae yaani dakika ya 56 kutumbukiza mpira wavuni na kuiweka Chelsea kuongoza kwa magoli 2-0.

Mpira ukaendelea kucheza mpaka dakika 12 baadae Taylor-Crossdale nae kufunga goli la tatu kabla ya kufunga tena goli la nne dakika ya 78, lakini kuonyesha kuwa bora zaidi, nyota huyohuyo alifunga tena goli lake la  tatu lakini likiwa ni goli la tano kwa timu ambapo mara hii alifunga kupitia kwa mkwaju wa penati na kuifanya Chelsea iwe kileleni.

Wakati mpira unaelekea kuisha, nyota wa Chelsea ambaye mara kadhaa amewai kuitwa kwenye kikosi cha timu ya wakubwa licha ya kutokupata nafasi, Dejon Sterling naye akaongeza goli jengine na kufanya kuondoka na ushindi huo mnono wa magoli 6-0 na kuifanya Chelsea ifudhu kucheza hatua ya nusu fainali. Lakini katika mchezo huo nyota wa Chelsea, Ethan Ampadu ambaye amekuwa akicheza kama mlinzi wa kati alikosekana, kusoma sababu hiyo, bonyeza hapa

No comments:

Post a Comment