Usiku wa leo, Chelsea itakuwa uwanjani kuwania nafasi ya kucheza hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya, ambapo itakuwa nchini Hispania kumenyana dhidi ya Barcelona. Kuelekea kwenye mchezo huo ambapo ili Chelsea ifanikiwe kuvuka na kucheza hatua ya robo fainali basi itahitaji ipate ushindi au ipate sare yoyote kuanzia sare ya 2-2.
Na kama ilivyoada kila siku ambapo Chelsea inashuka uwanjani kukuletea habari muhimu, basi na leo nakuletea habari muhimu kuelekea kwenye mchezo huo ambao leo unaenda kuweka historia mpya.
Habari Muhimu;
Chelsea; Kuelekea kwenye mchezo wa leo, Ethan Ampadu hatokuwepo kutokana na kutokufudhu kucheza mchezo huu, hajatimiza vigezo (Kama unataka kujua vigezo gani, bonyeza hapa) wakati kwa upande wa David Luiz naye ataendelea kuwa nje kutokana na kuuguza majeraha. Ross Barkley anaweza kujumuishwa kwenye kikosi cha leo.
Chelsea; Kuelekea kwenye mchezo wa leo, Ethan Ampadu hatokuwepo kutokana na kutokufudhu kucheza mchezo huu, hajatimiza vigezo (Kama unataka kujua vigezo gani, bonyeza hapa) wakati kwa upande wa David Luiz naye ataendelea kuwa nje kutokana na kuuguza majeraha. Ross Barkley anaweza kujumuishwa kwenye kikosi cha leo.
Kwa upande wa kinda, Callum Hudson-Odoi naye pia anaweza kuitumikia klabu yake ambapo mchezo wa akademi uliopita ambapo Chelsea ilimenyana dhidi ya West Ham, nyota huyu naye hakujumuishwa kutokana na kujiandaa na mchezo huu.
Barcelona; Kwa upande wa wababe hawa kuna uwezekano wa kiungo wao, Andres Iniesta akaukosa mchezo wa leo kutokana na kupata majeraha siku kadhaa zilizopita katika mchezo wa ligi kuu ingawa jana ilitoka taarifa kuwa nyota huyo amefanya mazoezi na wenzake mpaka mwisho na anaonekana kuwa imara tofauti na mwanzo. Ila klabu hii itakosa huduma ya kiungo wake, Phillipe Coutinho ambaye haruhusiwi kucheza kwa sasa kutokana na sheria za michuano zikimpiga panga kutokana na kuhusika katika mchezo wa kwanza.
Mechi zilizopita;
Chelsea; WDLLW
Barcelona; DWDWW
Chelsea; WDLLW
Barcelona; DWDWW
Rekodi; Mwaka 2012 ndio ulikuwa mwaka wa mwisho kwa timu hizi kukabiliana katika uwanja huuhuu wa leo wa Camp Nou, ambapo ulikuwa ni mchezo wa nusu fainali na ukaisha kwa sare ya 2-2 lakini Chelsea ikafanikiwa kufudhu kucheza fainali kutokana na mchezo wa kwanza kufanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Didier Drogba.
Muda; Saa 10:45 Usiku (saa 22:45) kwa saa za Afrika Mashariki


No comments:
Post a Comment