Mara baada ya kuibuka mzozo mkubwa juu ya kauli aliyoitoa mlinda mlango namba moja wa Chelsea, Thibaut Courtois juu ya kutamani kutua klabu ya Real Madrid ambayo imekuwa ikitajwa kwa muda mrefu kumhitaji mlinda mlango huyo raia wa Ubelgiji mwenye miaka 25 kwa sasa.
Thibaut Courtois alitoa maneno hayo akisema kiukweli moyo wake upo madrid na ataendelea kubaki Chelsea kwa kuwa hakuna maendelea ya karibu yanayoonyeshwa na wababe hao wa nchini Hispania, lakini moja ya wachambuzi wa soka na watu wa karibu wa mchezo huo nchini Hispania, Guillem Ballague anaamini mlinda mlango huyo hatojiunga na Real Madrid na badala yake atasaini mkataba mpya klabuni Chelsea.
Ballague anasema nyota huyo ni mchezaji anayejielewa na anajua nini anapaswa kufanya kwa wakati gani na anaamini hakuna kitakachoendelea juu ya nyota huyo kuondoka London na badala yake atasaini mkataba mpya ambapo inaeleweka Real Madrid inamtaka kipa huyo kama mbadala kama wakikosa kumnasa mlinda mlango wa klabu ya Manyumbu (Man utd), David de Gea.
COURTOIS KUBAKI CHELSEA?
Share This
Tags
# Chelsea Usajili
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Usajili
Labels:
Chelsea Usajili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment