Nyota wa klabu ya Chelsea, Eden Hazard bado anaendelea kuwakimbiza nyota wenzake huko nchini kwao Ubelgiji mara baada ya kutangazwa tena kuwa mchezaji bora wa ligi za nje kwa mwaka 2017 ambapo tunzo hiyo inaandaliwa na nchi ya Ubelgiji.
hii ni tunzo ya pili kwa nyota huyo kubeba ikiwakilisha ubora wa mwaka 2017, ambapo tunzo ya kwanza kuibeba ilikuwa ya mchezaji bora wa mwaka 2017 kwa Ubelgiji huku nafasi ya pili ikishikwa na mchezaji wa zamani wa Chelsea ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Mama site (Man city), Kevin De Bruyne ambaye pia amemaliza nafasi ya pili katika tunzo hizi zilizotolewa tena.
Kevin De ruyne anashika nafasi ya pili wakati Dries Mertens wa klabu ya Napoli akishika nafasi ya tatu na mshambuliaji mwengine wa zamani wa Chelsea, Romelu Lukaku ambaye kwa sasa anaichezea Manyumbu (Man utd) akishika nafasi ya nne.
Eden Hazard alipofanyiwa mahojiano juu ya tunzo hiyo alisema "Ni tunzo yangu ya kwanza ndani ya Ubelgiji, lakini pia sio tunzo ya mwisho." na alipoulizwa juu ya kura yake alimpigia nani alisema "Nilimpigia Mertens maana amekuwa bora sana huku akiwa anacheza nafasi ambayo hajaizoea. Kiasili sio mshambuliaji ila anacheza nafasi hiyo na ana mafanikio makubwa"
Hongera kwako Eden Hazard.
HAZARD AZIDI KUWASHA MOTO
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment