Wakati Chelsea FC ikiwa tayari ishafika nchini Hispania na sasa inajiandaa kumenyana dhidi ya Barcelona katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya, ambapo mchezo huo utachezwa usiku wa leo mishale ya saa 22:45 (kama unataka kupata habari muhimu kuhusu mchezo huu, bonyeza hapa), vijana wa Chelsea nao walikuwa uwanjani nchini hukohuko Hispania ambapo wao walikuwa wakicheza mchezo wa robo fainali dhidi ya vijana wa Real Madrid na wamefanikiwa kupata ushindi mnono huku wakiwa pungufu kwa mchezaji wake mmoja kupewa kadi nyekundu.
Real Madrid 2-4 Chelsea, ndivyo ulivyosomeka ubao wa matokeo mara baada ya mchezo huo kuisha. Real Madrid ndio walikuwa wa kwanza kupata goli ambapo dakika ya saba tu waliweza kuzifumania nyavu za Chelsea kupitia mpira wa adhabu uliopigwa na Oscar lakini goli hilo halikudumu maana liliishi kwa dakika nan tu kabla ya Luke McCormick kulichomoa goli hilo na kufanya matokeo kuwa 1-1. Dakika kadhaa tena, McCormick akaifungia Chelsea goli la pili mara baada ya mlinzi wa Real Madrid kupiga mpira ovyo na kumgonga Redan kabla haujakutana na McCormick na kufunga goli kiulaini akibakia na mlinda mlango na kufanya matokeo kuwa 1-2.
Muda huu ilikuwa ni zamu ya Redan kufunga goli murua na kuipatia Chelsea uongozi wa kuongoza mchezo huo na kufanya matokeo kuwa 1-3 na kufanya matokeo kuwa hivyo mpaka kufikia muda wa mapumziko.
Kipindi chapili ndicho kilikuwa kigumu kwa Chelsea mara baada ya Real Madrid kuchomoa goli jengine na kufanya matokeo kuwa 2-3, lakini kipindi hicho kilionekana kuwa kigumu zaidi mara baada ya nyota wa Chelsea kupata kadi nyekundu na ksababisha kucheza tukiwa puungufu, ugumu mwengine ukaja mara baada ya mlinzi wake, Ethan Ampadu kupata majeraha na kushindwa kuendelea na mchezo mpaka alipotolewa na nafasi yake kuchukuliwa na George McEachran, mabadiliko hayo yalifanyika dakia ya 80.
Chelsea ikaonekana inajilinda sana kutokana na Madoxx kuonyeshwa kadi nyekundu na mpaka zinatimia dakika 90, Chelsea ilikuwa bado ipo mbele kwa ushindi wa mabao 2-3. Mwamuzi akaamuru ziongezwe dakika tano, ambapo kwa safari hii, ilikuwa ikitumia mfumo wa 4-4-1 ambapo kwa nafasi ya ushambuliaji ikiongozwa na StClair ambaye hakufanya makosa mara baada ya Real Madrid kufanya makosa na kuifanya Chelsea kupata goli jengine na kufanya mchezo kuisha kwa Chelsea kushinda 2-4.
Kwa matokeo hayo, kunaifanya Chelsea kufanikiwa kutinga nusu fainali na itacheza dhidi ya FC Porto siku ya tarehe 20-Aprili.
Hongereni vijana..
CHELSEA YAPATA USHINDI MNONO, RATIBA YA NUSU FAINALI YATOKA
Share This
Tags
# Chelsea Habari
# Chelsea Youth
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Youth
Labels:
Chelsea Habari,
Chelsea Youth
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment