WILLIAN AIPA CHELSEA MBINU YA KUIKABILI Barcelona - Darajani 1905

WILLIAN AIPA CHELSEA MBINU YA KUIKABILI Barcelona

Share This
Kuelekea mchezo wa leo usiku ambapo Chelsea inashuka uwanjani kumenyana dhidi ya Barcelona ili kukamilisha mchezo wa marudiano mara baada ya mchezo wa kwanza kuisha kwa suluhu ya 1-1, huku goli la Chelsea likifungwa na nyota raia wa Brazil, Willian Borges ambaye kwa sasa amekuwa kwenye kiwango cha hali ya juu.

Nyota huyo ametoa neno na kueleza kwa jinsi gani Chelsea ikicheza mchezo huo itaweza kuondoka na matokeo mazuri yatakayoifanya ifanikiwe kufudhu kucheza hatua ya robo fainali.

Kwanza ilikuwa ni jambo zuri kurudi katika hali ya ushindi maana inatupatia kujiamini dhidi ya Barcelonsa. Katika mpira, unapopata ushindi katika mchezo fulani basi nawe unapata kujiamini ili kuukabili vyema mchezo ujao. Na sasa tuna hali hiyo ya kujiamini kuelekea kwenye mchezo huu"

"Kucheza dhidi ya Barcelona sio jambo jepesi. Uwanja wa kule ni mkubwa na tunategemea kukutana na mchezo mgumu lakini kama navyofikiria, kama tukicheza kama tulivyocheza mchzo wa kwanza kule Stamford, basi tutaweza kufudhu"

"Inatakiwa tuwe na nguvu na kupambana pamoja hata tukiwa hatuna mpira maaba Barcelona mara zote wamekuwa ni timu ya kumiliki mpira. Kwenye mchezo huu kama tukipata mpira basi inabidi tuwe na uwezo mkubwa wa kufanya maamuzi sahihi. Na tujitahidi tusifanye makosa haswa kwenye pasi zetu na tunatakiwa tuwe wahatari haswa tunapolifikia lango lao. Kama tukiingia kwenye mchezo tukiwa na mbinu huu naamini tutafanya jambo la kipekee" alisema winga huyo ambaye katika mchezo uliopita dhidi ya  Crystal palace aliifungia goli Chelsea katika ushindi wa mabao 2-1.

No comments:

Post a Comment