UEFA; FT, Barcelona 3-0 CHELSEA - Darajani 1905

UEFA; FT, Barcelona 3-0 CHELSEA

Share This
Ni kutokuwa makini na kutokuwa na bahati ndivo vitu ilivyokosa Chelsea katika mchezo huu ambapo imepoteza na kuondoshwa kwenye michuano hii ya ligi ya mabingwa barani Ulaya mara baada ya kuruhusu magoli 3-0 ikiwa ugenini nchini Hispania.

Mkwaju wa mpira wa adhabu uliopigwa na Marcos Alonso katika dakika ya 45 unagongwa mwamba na kutoka nje, ambapo kama angefanikiwa kufunga basi angefanya matokeo kuwa 2-1 mpaka kuelekea mapumziko, lakini ndio kama nilivyoanza kusema bahati haikuwa kwetu licha ya kuruhusu magoli mawili yaliyofungwa na Lionel Messi na Dembele.

Kipindi cha pili, Chelsea iliingia uwanjani ikiwa na lengo la kutafuta suluhu ya 2-2 ili ifanikiwe kufudhu kucheza hatua inayofata ambapo ilifanikiwa kulisakama lango la wapinzani, huku pia ikitengeneza nafasi nyingi, lakini nafasi hizo zikaishia kuwa chakula kwa walinzi wa Barcelona na kufanya kuziondosha kiurahisi.

Antonio Rudiger naye akapigwa kichwa kuonganisha mpira wa kona na kushuhudia mpira ukigonga mwamba na kutokuwa na madhara. Chelsea tulikosa bahati. Willian na Hazard walijitahidi kwa kiasi kikubwa kutengeneza mashambulizi lakini umakini nao ulikosekana mpaka mpira unaisha, Barcelona 3-0 Chelsea. Ambapo goli la tatu la Barcelona lilifungwa na Lionel Messi.

Kikosi cha Chelsea; Thibaut Courtois, Cesar Azpilicueta, Andreas Christensen, Antonio Rudiger, Victor Moses (Davide Zappacosta), N'golo Kante, Cesc Fabregas, Marcos Alonso, Eden Hazard (Pedro) , Willian, Olivier Giroud (Alvaro Morata)

Wachezaji wa akiba; Willy Caballero, Davide Zappacosta, Gary Cahill, Tiemoue Bakayoko, Emerson Palmieri, Pedro, Alvaro Morata

No comments:

Post a Comment