Chelsea itashuka uwanjani kesho kumenyana dhidi ya Barcelona katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa barani Ulaya maarufu kama UEFA Champions League (UCL) ambapo Chelsea itasafiri kuifata klabu hiyo nchini Hispania.
Kuelekea kwenye mchezo huo, nyota wa Chelsea, Cesc Fabregas ameeleza mpango ambao kama ukitumika basi Chelsea itaweza kumzuia mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi lakini pia na kuweza kuishinda klabu hiyo na kufanikiwa kufudhu kucheza hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
"Kama nikiwa na bahati ya kucheza mchezo huo, najua ni kweli wamekuwa na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira kwenye maeneo mengi uwanjani, najua kumzuia (Messi) ni ngumu sana, lakini nitajaribu kufanya jambo lolote linalowezekana ili asijihisi yupo huru na hatimaye ashindwe kuifanya klabu yake na wenzake washindwe kucheza vizuri"
"Namuona Messi kama ni mpinzani anayetaka kushinda, lakini nami pia nahitaji hilohilo, kushinda. Tupo katika timu tofauti na kila mchezaji anataka litokee zuri kwa klabu yake. Nafahamu inatakiwa muda wote muheshimiane"
"Sioni tatizo kucheza dhidi ya marafiki zangu. napenda kuhusisha hisia zilizochanya mara zote. Nilifanya hivyo nilipokuwa Arsenal, na sasa nipo Chelsea. Nimekuwa najihisi kuwa sawa katika vipindi vyote . Hainisumbui kucheza dhidi ya klabu yangu ya zamani, dhidi ya marafiki zangu, ila inanichangamsha. Na kama nilivyosema, kuwa nachangamka sihitaji mtu yoyote awe na mashaka katika hilo kwamba nahitaji klabu yangu ipate kitu kilichobora. Kiukweli inanichangamsha sana" alisema nyota huyo ambaye kabla ya kutua Chelsea alikuwa mchezaji wa klabu hiyo haswa pia ukilinganisha Hispania ndio nchi yake.
Chelsea ili ifanikiwe kuvuka na kucheza hatua ya robo fainali basi itahitaji ushindi wowote au hata ikipata sare ya magoli kuanzia 2-2 na kuendelea basiitakuwa imefudhu kucheza hatua inayofata. Lakini kama mchezo utaisha kwa sare ya 1-1 basi zitaongezwa dakika 30 kutokana na mchezo wa kwanza uliisha kwa sare hiyo ya 1-1.

No comments:
Post a Comment