Nyota wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba ambaye kwa sasa ni mchezaji na mmiliki wa klabu ya soka ya nchini Marekani, Phoenix Rising ambayo pia ni mmoja kati ya wamiliki wa klabu hiyo ametangaza rasmi muda wa kustaafu soka ambapo jumapili alitoka kutimiza miaka 40.
"Ni jambo zuri kwangu kucheza soka, nilianza kufanikiwa nikiwa nna umri mkubwa na kufanikiwa kufikia amafanikio makubwa. Ninajisikia raha napocheza soka. Nafurahishwa sana na nafasi niliyokuwa nayo kwa sasa kama mmiliki-mchezaji. Nimezungukwa na wachezaji wenye umri mdogo na napenda kuhamisha ule uzoefu wangu kutoka kwangu na kuwapatia. Lakini msimu huu ni wa mwisho kwangu, nina miaka 40 sasa" alisema gwiji huyo ambaye aliisaidia Chelsea kushinda mataji mengi kama ya ligi kuu Uingereza, makombe ya FA na makombe ya ligi lakini pia aliisaidia kushinda taji la klabu bingwa Ulaya.
DROGBA ATANGAZA TAREHE YA KUSTAAFU SOKA
Share This
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment