MARCOS ALONSO KUTOA ZAWADI KWA MASHABIKI - Darajani 1905

MARCOS ALONSO KUTOA ZAWADI KWA MASHABIKI

Share This
Kupitia mtandao wa Instagram, nyota wa Chelsea, Marcos Alonso au mjukuu wa Mendoza ametuma ujumbe kuhusu kukaribia kwake kutimiza wafuasi (followers) milioni 1 katika mtandao huo.

Nyota huyo ametuma ujumbe akionyeshwa kufurahishwa na watu wanaomfatilia kwa kuonyesha kumjali siku baada ya siku na hivyo ameandaa zawadi kwa hao watu wanaomfatilia kwamba endapo akitimiza wafuasi milioni 1 basi atatoa zawadi ya fulana zake anazozitumia kama mchezaji wa Chelsea ambapo zitakuwa fulana tano pamoja na zawadi ya jozi (pair) tano za viatu.

Ili kupata maelekezo jinsi ya kumfatilia nyota huyo, basi mfatilie katika mtandao huo ili uweze kujishindia zawadi hizo. Mpaka sasa ana wafuatiliaji 977k (977,000+)

No comments:

Post a Comment