Kama Chelsea ikifanikiwa kushinda michezo nusu fainali pamoja na fainali ya michuano hiyo basi itafanikiwa pia kuweka rekodi ya kutwaa taji hilo mara tano mfululizo ambapo mpaka sasa imeshashinda michuano hiyo mara nne huku ikifanikiwa kuweka rekodia kufika hatua ya nusu fainali mara tisa mfululizo katika kombe hilo la FA.
Lakini pia hii ni mara ya pili mfululizo, Chelsea inamenyana dhidi ya Birmingham ambapo mwaka jana mwezi Januari, Chelsea iliibamiza klabu hiyo katika hatua ya raundi ya nne kwa magoli 5-0 ambapo magoli ya Chelsea yalifungwa na Mason Mountambaye alifunga magoli matatu na kwa sasa anaichezea klabu ya Vittese kwa mkopo, Reece James pamoja na Cole da Silva.

No comments:
Post a Comment