Kanla ya kuondoka alihakikisha anajifungia pingu klabuni Chelsea kwa kusaini mkataba mpya wa miaka mitano, akafika Stoke city ambayo alijiunga nayo kwa mkopo hiyo ilikuwa katika dirisha kubwa la usajili lililopita. Ni Kurt Zouma.
Nyota huyo ametoa taarifa juu ya maisha yalivyo huko alipo akicheza kwa mkopo, "Watu wanajua kwamba nipo hapa kwa mkopo wa msimu mmoja na haijalishi ni nini kitatokea mara baada ya msimu huo kuisha, naamini Stoke itaendelea kuwepo ligi kuu. Lengo langu haswa ni kurudi Chelsea lakini muhimu ni kufanya kwanza vizuri nikiwa bado nipo hapa. Sihitaji niende chini na kiwango changu kushuka"
"Lengo langu ni kurudi Chelsea na kupata nafasi ya kucheza. Wamenipa nafasi ya kutoka kwa mkopo na niliongea na kocha wangu ambaye alikubali hilo litokee na walinisaidia kutoka kwenye majeruhi na wakanisaidia pia kutafuta klabu nitakayoweza kupata nafasi ya kucheza" alisema nyota huyo raia wa Ufaransa.
Kurt Zouma alisajiliwa akitokea klabu ya St.Etienne ya nchini Ufaransa, na amekuwa akitajwa kama moja ya walinzi watakaokuja kufanya vizuri klabuni Chelsea haswa ukilinganisha umri wake wa sasa bado ni mdogo na ana nafasi kubwa ya kurejea na kuonyesha makubwa. Kwa sasa ana miaka 23.

No comments:
Post a Comment