Kocha wa Chelsea, Antonio Conte aliwai kuingia katika vita ya maneno kati yake dhidi ya kocha wa zamani wa Chelsea ambaye kwa sasa anaifundisha klabu ya Manchester united, Jose Mourinho ingawa kwa sasa malumbano hayo yakionekana yamefifia kama sio kuisha kabisa.
Hivi karibuni kuliwai kuchukuliwa video katika mkutano wa waandishi wa habari pamoja na kocha wa Chelsea, Antonio Conte ambapo mwandishi mmoja kutoka nchini Italia aliwasilisha ujumbe wa video pamoja na fulana ya Manchester united kwa kocha wa Chelsea akisema ujumbe huo ulitoka kwa Mourinho ambapo alisema sababu ya vitu hivyo kumfikia yeye ni kwamba alilenga kuomba msamaha na kutaka kumaliza tofauti kati yake na Conte. Kama unataka kuisoma habari hiyo, bonyeza hapa
"Sitaki kuliongelea hilo, jambo muhimu ni kwamba Antonio Conte na mimi tumefanya jambo sahihi, kulikuwa na matatizo hapo kabla ila tumeyamaliza na tumeshasahau na kudhihirisha kwamba Mourinho ni Mourinho na Conte ni Conte. Yeye (Conte) ni kocha wa Chelsea na mimi ni kocha wa United" alisema Jose Mourinho alipoulizwa juu ya mahusiano yake na kocha wa Chelsea, Antonio Conte.

No comments:
Post a Comment