Kocha wa Chelsea, Antonio Conte huwa na kawaida ya kufanya mkutano kila baada ya siku kadhaa kabla ya Chelsea kushuka uwanjani, na leo amefanya mkutano huo kuelekea mchezo wa kesho ambapo Chelsea itakuwa nyumbani kumenyana dhidi ya Hull city katika michuano ya kombe la FA kwa hatua ya raundi ya tano.
Katika mkutano wa leo kuna tukio la kushangaza lilitokea, mara baada ya mmoja wa waandishi wa habari ambaye anatokea kwenye chombo cha habari cha nchini Italia, alinyanyuka wakati mahojiano yakiwa yanaendelea ambapo kocha Antonio Conte alikuwa akiyajibu.
Mwandishi huyo aliinuka na kumfata kocha Antonio Conte na kumwambia samahani kuna ujumbe kwa ajili yako na kumuonyesha video iliyokuwa kwenye simu ambapo ilikuwa ikimuonyesha kocha Jose Mourinho ambaye ni kocha wa Manyumbu (Man utd) ambaye alishawai kuwa kocha wa Chelsea kwa vipindi viwili tofauti.
Hiyo video aliyokuwa anaonyeshwa kocha Antonio Conte ilisikika kwa maneno mengi lakini jambo kubwa lililokaririwa ni sauti iliyoaminika kuwa ya kocha Mourinho ikisema anataka urafiki kati yake na kocha Antonio Conte urudi kama zamani na haina haja ya kuchukiana kutokana na maneno waliyowai kurushiana hapo kabla huku ikisikika kuwa kocha huyo anatamani ata klabu zao zitakapomenyana tarehe 25-Februari basi wawe karibu na kutokuonyesha chuki zao.
Baada ya kocha Antonio Conte kuonyeshwa ujumbe huo, hakujibu kitu zaidi ya kubaki anatabasamu tu.
Lakini kama haitoshi, kocha huyo akasema ametuma zawadi kwa kocha huyo ambayo ina ujumbe muhimu kwake, na anaomba aipokee zawadi hiyo. Na ndipo huyo mwandishi wa habari akaichukua iyo zawadi ambayo ni fulana au jezi ya klabu ya Manyumbu (Man utd) iliyoandikwa jina la Antonio Conte ikiwa na namba moja na ikiwa imesainiwa na Jose Mourinho.
Kocha Jose Mourinho amekuwa akisifika kwa kuwa na kejeli na ugomvi w maneno kwa makocha wengi, ambapo kwa ugomvi wa maneno na Antonio Conte ulianza msimu huu kuelekea mwisho wa mwaka uliopita. Na kuna makala niliwai kukuletea kuhusu kocha huyu, na hili linalotokea leo alishawai kulisema. Je unataka kujua alisema nini kabla ya siku ya leo? bonyeza hapa
Lakini kwa upande wa kocha Antonio Conte hakusema lolote zaidi ya kumwambia mwandishi huyo abaki na ile fulana na maswali yakaendelea kutokana na msimamizi wa mikutani ya waandishi wa habari klabuni hapo kuamuru tendo lile lisitishwe na mkutano uendelee.
No comments:
Post a Comment