Chelsea iliweka rekodi mpya kwa kuchezesha wachezaji wawili katika mchezo mmoja ambao walizaliwa miaka ya 2000 na kuja juu, ambapo iliwachezesha Ethan Ampadu pamoja na Callum James Hudson-Odoi ambao wote wamezaliwa mwaka 2000. Kwa Hudson-Odoi lilikuwa ni jambo kubwa kwake maana Chelsea kwake ni klabu anayoifanyia kazi kama mchezaji wa kulipwa, lakini pia ni klabu anayoshabikia.
Lakini kabla ya kucheza mchezo wake wa kwanza, nyota huyo aliongea na kocha Antonio Conte kabla ya kumpa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha wakubwa akitokea kwenye kikosi cha vijana.
"Kocha aliongea namimi, kabla hata hajanipa muda wa kucheza katika kikosi cha wakubwa. Aliniambia natakiwa kupambana na kuonyesha ukomavu wangu katika kucheza."
"Kiukweli, nilitakiwa kuwa mtulivu maana mi bado mdogo, lakini nilipopata nafasi ya kucheza mchezo wangu wa kwanza nilijua sasa ni muda wangu wa kuwa uwanjani, na kukionyesha kile nachotakiwa kukifanya. Na kuonyesha kuwa sasa nipo tayari."
"Wachezaji wengine wamekuwa wakinipa msaada mkubwa sana. Wananifanya nijiamini na mara zote wananishauri na wanataka nifanye vitu bora na vikubwa. Haijalishi kwa kiasi gani unakosea, bado wanakufata na kukwambia najua unaweza kufanya zaidi ya hivi, na inatakiwa ufanye katika ubora. Hawakufanyi ujihisi una makosa, ila wanakufanya ujihisi kuwa unaweza kila kitu" alisema nyota huyo aliyeiongoza timu ya Chelsea ya vijana kufanya makubwa.
HUDSON-ODOI AELEZA ALICHOAMBIWA NA KOCHA ANTONIO CONTE
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment