ALICHOKISEMA ANTONIO CONTE KUELEKEA CHELSEA vs HULL CITY - Darajani 1905

ALICHOKISEMA ANTONIO CONTE KUELEKEA CHELSEA vs HULL CITY

Share This
Kama ilivyokawaida ya kochaAntonio Conte kufanya mkutano kabla ya siku ambayo Chelsea itashuka uwanjani kupambana dhidi ya klabu fulani,na leo pia amefanya mkutano huo na waandishi wa habari lakini hii ya leo ikiwa tofauti ikifanyika siku ya Alhamisi ikiwa na tofauti ilivyozoeleka kocha huyo kufanya mkutano huo kila ijumaa. Imetokea hivi kwa maana kesho siku ya ijumaa ndio Chelsea itakuwa ikishuka uwanjani kupambana dhidi ya Hull city katika mchezo wa kombe la FA kwa raundi ya tano, ambapo mshindi atakayeshinda hapo atafanikiwa kufudhu kucheza hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Katika mkutano huo, amefanyiwa mahojiano juu ya mambo mengi, ila hapa nakuletea baadhi;

Alipoulizwa juu ya jinsi gani anaichukulia michuano hiyo, na kama anaipa kipaumbele gani, kocha huyo alisema "Kwetu kila michuano ina kipaumbele, kama tulivyoonyesha kipaumbele katika michuano ya Carabao mpaka tukaishia nusu fainali na vivyo hivyo tutakavyotia nguvu katika michuano hii"

Alipoulizwa juu ya wachezaji gani watakuwa majeruhi na kuukosa mchezo huo, kocha Antonio Conte alisema "David Luiz, Tiemoue Bakayoko na Ross Barkley hawatoweza kucheza mchezo huu lakini kabla ya mchezo huo tutatakiwa kujihakikishia mambo mawili"

Kuhusu maendelea ya timu anayaonaje kuelekea kwenyewingi ya klabu bingwa Ulaya, kocha Antonio Conte alijibu "Tuna wiki mbili ambazo tutakuwa kwenye michezo migumu, tuna pango kama klabu tumejianzishia katika kukabiliana na wiki hizo zenye michezo migumu"

Juu ya maamuzi aliyoyafanya ya kuwapumzisha wachezaji na benchi la ufundi kwa siku tatu kabla ya mchezo uliopita dhidi ya West Bromwich, kocha Antonio Conte alijibu "Ulikuwa ni uamuzi sahihi kuuchukua ili kupumzika, kipindi kilichopita hatukupata nafasi ya kupumzika"

Alipoulizwa juu ya hatma yake klabuni Chelsea, na kama anajiona ataendelea kuwa kocha wa Chelsea au laah, kocha Antonio Conte alijibu "Nadhani tuachane na hii maada, maana ni kila wiki naulizwa swali hili. Muhimu kwa sasa ni kuongelea kuhusu timu na michezo inayotukabili"

Alipoulizwa juu ya uwepo wa Alvaro Morata na Olivier Giroud, ni nani atakuwa kipaumbele, kocha Antonio Conte alisema "Morata ni mchezaji anayeonesha ukomavu mkubwa. Kuwa na watu wawili wa aina hii ni jambo zuri kwa timu, maana inakuwa vyema kwa kila nafasi kukawa na ushindani. Giroud ni mchezaji mzuri mwenye nguvu, atatusaidia sana kwenye kampeni yetu mpaka mwishoni mwa msimu"

Kuhusu mchezaji wa Hull city, Ryan Mason ambaye amestaafu soka mara baada ya kugongana kichwa na mlinzi wa Chelsea, Gary Cahill mwezi Januari mwaka jana, kocha Antonio Conte alisema "Ni habari mbaya na za kusikitisha kupata. Mason alikuwa mchezaji muhimu na inaikitisha kuona anaachana na soka akiwa ndio kwanza ana uri mdogo kabisa (ana miaka 26). Wachezaji katika timu wanamuombea baraka na kufanikiwa na kumpa pole yeye pamoja na familia yake"

Alipoulizwa juu ya mashabiki wa Chelsea, kocha Antonio Conte alisema "Nalishukuru sana kwa wanalolifanya mashabiki, mimi pamoja na klabu tunajitahidi kupambana ili kuwafanya wajivunie timu yao, na wanaliona hilo na ndio maana wanatupa nguvu mara zote"

Kuhusu Ampadu na Callum Hudson-Odoi kupata nafasi katika mchezo huo, kocha Antonio Conte alisema "Niliwapatia nafasi katika michuano ya Carabao, ni jambo zuri kuwa nao. Hao ni kati ya nyota bora katika kikosi cha Chelsea cha vijana, sio hao tu, kuna mdogo wa Chalobah (Trevoh Chalobah), kuna Sterling na Scott wote watapata nafasi maana naamini Chelsea ya baadae itakuwa bora zaidi kupitia hawa"

Kocha Antonio Conte akamaliza mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa mazoezi wa Chelsea unaoitwa Cobham Stadium.


No comments:

Post a Comment