Kocha Benitez amewaambia mashabiki wa klabu hiyo kwamba huu ndio muda wa kula mafanikio na ubora wa nyota huyo maana ifikapo dirisha kubwa la usajili nyota huyo atarudi kwenye klabu yake ya Chelsea
"Ni zaidi ya ubora na kasi yake, ni mchezaji anayecheza kwa kujiachia na kujipa nafasi akiwa na mpira. Anafanya kila mchezaji bora anapaswa kukifanya, anatoa pasi ndefu, anapiga faulo. Ni mchezaji anayecheza kwa kujiamini'
"Sina uhakika kama kutakuwa na uhakika wa kuendelea kubaki nae mara baada ya msimu kuisha, nadhani kwa sasa tunatakiwa kuupata ule ubora wake wakati yupo hapa" alisema kocha huyo ambaye aliifundisha Chelsea na kuisaidia kushinda taji la Europa.

No comments:
Post a Comment