Habari muhimu kuelekea Chelsea vs Liverpool - Darajani 1905

Habari muhimu kuelekea Chelsea vs Liverpool

Share This

Chelsea inashuka uwanjani katika mchezo wa ligi kuu Uingereza jioni hii ya leo ambapo inahitaji ushindi na kuvuna alama tatu ili kujiweka sawa kwenye msimamo wa ligi kuu nchini humo. Itakuwa nyumbani Stamford Bridge ili kucheza mchezo wake wa ligi kuu dhidi ya Liverpool, mchezo ambao kama ikifanikiwa kupata ushindi basi itafikisha alama 69 huku ikiwa imecheza michezo 36 na kubakiza michezo miwili ili msimu huu umalizike.

Kuelekea kwenye mchezo huo muhimu zaidi kwa Chelsea, hapa nakuletea habari muhimu kuelekea kwenye mchezo huo.

Habari muhimu;
Chelsea; Inashuka katika mchezo huu huku ikiendelea kukosa huduma ya mchezaji wake, David Luiz ambaye anaendelea kuuguza majeraha yake wakati ikiendelea pia kukosa huduma ya kinda Ethan Ampadu ambaye mchezo wa fainali ya kombe la FA kwa vijana chini ya miaka 18 ambapo Chelsea iliibuka mabingwa dhidi ya Arsenal kinda huyo aliishia kuutazama mchezo huo akiwa kama shabiki.

Marcos Alonso, ambaye ni mlinzi wa kushoto anayecheza pia kama winga (left wing-back) anamaliza adhabu yake ya kufungiwa michezo mitatu ambapo aliikosa mchezo wa nusu fainali ya kombe la FA dhidi ya Southampton pamoja na michezo miwili ya ligi kuu ambayo ni dhidi ya Burnley na dhidi ya Swansea.

Liverpool; Hawa majamaa watashuka uwanjani huku ikiwakosa wachezaji wake Joel Matip, Emre Can, Adam Lallana na Alex Oxlade-Chamberlain ambao wanauguza majeraha.

Mwamuzi; Anthony Taylor ndiye mwamuzi wa mchezo wa leo ambapo alikuja duniani tarehe na ni mzaliwa wa jiji la Manchester

Rekodi; Toka mwaka 1985 mpaka mwaka 1990, Chelsea ilifululiza kupata ushindi dhidi ya Liverpool katika michezo 10.

Michezo iliyopita;
Chelsea: LDWWW
Liverpool:

Muda; Saa 06:30 Jioni (Saa 18:30) kwa saa za Afrika Mashariki (EAT)

No comments:

Post a Comment