Vijana wa Chelsea watwaa ubingwa wa ligi kuu, sasa rasmi klabu bingwa - Darajani 1905

Vijana wa Chelsea watwaa ubingwa wa ligi kuu, sasa rasmi klabu bingwa

Share This

Kikosi cha vijana wenye umri chini ya miaka 18 cha Chelsea maarufu kama Chelsea U18s hapo juzi walifanikiwa kupata ushindi mnono wa magoli 0-3 wakiwa ugenini dhidi ya kikosi cha vijana cha Manchester united, ushindi uliomaanisha kikosi cha vijana cha Chelsea kilijitangaza rasmi kuwa mabingwa kwa mara nyengine kwa taji hilo la vijana kwa ligi kuu Uingereza.

Kwanza kabla ya kuendelea napenda kuomba radhi kwa kushindwa kukuletea taarifa hii kwa muda wa muafaka ambapo imesababishwa na sababu zilizo nje ya uwezo wangu.

Baada ya kukuomba radhi acha niendelee kukupa taarifa za mabingwa hao wanaonolewa na aliyewai kuwa mchezaji wa zamani wa Chelsea ambaye kwa sasa ndie kocha wa kikosi hicho cha vijana, Jody Morris ambapo amefanikiwa kukiongoza kikosi hicho kushinda taji lake la nne kwa msimu huu.

Dujon Sterling, Billy Gilmour na Tariq Lamptey ndio walikuwa wafungaji katika magoli hayo matatu ambayo yanaisaidia tena kikosi hicho cha vijana kufudhu kucheza michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa msimu ujao ambapo kwa msimu huu wamefanikiwa kufika fainali ya michuano hiyo ambapo walipoteza mbele ya Barcelona huko jijini Nyon nchini Switzerland.

Mataji manne ambayo wameshinda mpaka sasa ni pamoja na kombe la FA kwa vijana maarufu kama FA Youth Cup, kombe la ligi kuu kwa kanda yq kusini (the southern section of the Under-18 Premier League) pamoja na kombe la ligi maarufu kama the Under-18 Premier League Cup ukionganisha na taji la ligi kuu Uingereza ambalo ndio hili walilolitwaa kwa kuibamiza Manchester united.

Ubingwa huu unamaanisha kikosi hiki kinafudhu kucheza michuano ya klabu bingwa Ulaya kwa msimu ujao hata kama kikosi cha wakubwa cha Chelsea kitashindwa kufudhu kucheza michuano hiyo msimu ujao ambapo kwa kawaida kikosi cha wakubwa kikifudhu kucheza klabu bingwa basi inaipa tiketi kikosi cha vijana nacho kushiriki.

No comments:

Post a Comment