UFAFANUZI KUHUSU TUNZO ZA FIFPRo WORLD XI - Darajani 1905

UFAFANUZI KUHUSU TUNZO ZA FIFPRo WORLD XI

Share This
Sisi kama mashabiki wa Chelsea, tunachukua fursa hii kwa kuwapongeza nyota wa Chelsea Ladies kwa kufanikiwa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha tunzo za FIFPro  Womens World XI ambapo nyota watatu wa klabu ya Chelsea Ladies wamefanikiwa kuingia kwenye kinyanganyiro hicho.

Karen Carney (wa kwanza kushoto) ambaye anacheza nafasi ya kiungo, Hedvig Lindahl (wa kwanza kulia) ambaye ni mlinda mlango na Millie Bright (wa katikati) mwenye uwezo wa kucheza kama beki ambapo kutafanyika uchaguzi ili kuwachagua wachezaji kumi na moja watakaoingia kwenye kikosi hicho cha FIFPRo kwa mwaka 2017.

Shindano hili linahusisha wachezaji 55 kutoka mataifa mbalimbali duniani yaliyo chini ya chama cha soka cha dunia, FIFA ambapo hapa inahusisha wale wachezaji wanaocheza soka la hadhi ya juu (professional) ambapo kutafanyika uchaguzi ili kuwachagua wachezaji 11 ambao wao ndio watakuwa wamefanya vizuri kwa mwaka 2017 ambapo kikosi hicho kitatangazwa rasmi Alhamisi ijayo siku ya tarehe 8-Marchi ambapo pia ndio itakuwa siku ya wanawake duniani.

No comments:

Post a Comment