MKONGWE WA CHELSEA AMTETEA ANTONIO CONTE - Darajani 1905

MKONGWE WA CHELSEA AMTETEA ANTONIO CONTE

Share This
Chelsea itasafiri tena mwisho wa wiki hii mpaka kwenye jiji la Manchester ambapo huko watashuka uwanjani kukimenya dhidi ya klabu inayomilikiwa na tajiri wa kiarabu, Sheikh Mansour, klabu ya Manchester city katika mchezo wa raundi ya 29 ya michuano ya ligi kuu Uingereza. Kuelekea kwenye jiji hilo, bado kuna kumbukumbu ya mchezo uliopita ambapo Chelsea ilikuwa kwenye jiji hilohilo kumenyana dhidi ya Manchester united katika mchezo wa ligi kuu, ambapo mchezo huo ulichezwa wiki iliyopita na kuisha kwa Chelsea kupoteza kwa magoli 2-1.

Ambapo matokeo hayo yalionekana kuwakera mashabiki wa Chelsea huku wengi wakiamini kupoteza kwa mchezo huo ni kutokana na mabadiliko aliyoyafanya kocha wa Chelsea, alipomtoa Eden Hazard dakika ya 73 na kumwingiza Pedro, huku wakati nyota huyo anatolewa matokeo yalikuwa 1-1, na dakika mbili baadae Chelsea ikafungwa goli la pili na kuwafanya kupoteza mchezo huo huku wengi wakiamini kumtoa Eden Hazard kuliwapa furaha wachezaji waupinzani kutokana na kupata uhuru zaidi.
Moja kati ya watu waliolaumu kufanyiwa mabadiliko kwa nyota huyo, ni mbelgiji mwenzake katika kikosi cha timu hiyo, mlinda mlango Thibaut Courtois ambaye alisema katika mchezo kama ule hakuona sababu ya kumtoa Hazard maana anaweza akasababisha madhara muda wowote kutokana na ubora wake.

Lakini gwiji wa soka wa Chelsea, Dennis Wise amekataa kuzipeleka lawama zake kwa kocha Antonio Conte juu ya mabadiliko hayo na kusema anaamini kila mchezaji bado ana imani na kocha huyo na hakuna mchezaji anayependa kocha huyo kuondoka klabuni hapo na hata kufanya mabadiliko kwa mchezaji huyo alikuwa na lengo la kiufundi na kiuanamichezo.

Kocha Antonio Conte mwenyewe aliulizwa juu kwanini aliamua kufanya mabadiliko hayo, na mwenyewe alisema aliamua kufanya mabadiliko hayo ili aweze kuleta uwiano sawa katika safu ya ushambuliaji na safu ya ulinzi akimini nyota huyo hakuwa sawa kuendelea kutoka na kuchoka kwake.

No comments:

Post a Comment