Kumekuwa na sintofahamu inayoendelea klabuni Chelsea huku moto mkubwa ukitajwa kufukuta chini kwa chini. Haijajulikana kama siku ukilipuka utamuunguza nani lakini kwa asilimia kubwa kocha Antonio Conte huenda akaungua kutokana na moto huo ambao kikubwa unahusisha usajili.
Kumekuwa na malalamiko mengi yakiendelea juu ya usajili huo, mara baada ya mchezo wa juzi dhidi ya Arsenyani (Arsenal), kocha Conte alieleza masikitiko yake kutokana na kutopewa nafasi katika maswala ya usajili klabuni hapo huku majukumu hayo akiachiwa mwanamama, Marina Glanovskaia ambaye ni mmoja ya viongozi klabuni hapo lakini pia ni mtu wa karibu wa mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich.
Kocha Antonio Conte analalamika mawazo yake juu ya usajili klabuni hapo kutopewa nafasi huku anaowapendekeza wasajiliwe hawasajili.
"Ana haki ya kulalamika. Kutokana kwa muda aliofika klabu imepata fungu kubwa lakini haionyeshi kutamani kupata wachezaji wenye hadhi kubwa. Chelsea imecheza dhidi ya Arsenal mara nying, karibu mara tano na mara ya sita kwenye fainali ya FA msimu uliopita, na kote huko imeshindwa kupata mafanikio au matokeo chanya" alisema mchambuzi wa michezo, Martin Keown ambaye aliwai kuwa mchezaji wa Arsenyani.
Chelsea imepata fungu kubwa kwa misimu hii ilipokuwa chini ya kocha Antonio Conte mara baada ya kusaini mkataba na kampuni ya vifaa vya michezo ya Nike, pamoja na kusaini mkataba wa udhamini ya Carabao lakini pia kupata fungu kubwa kama bingwa wa ligi kuu Uingereza kwa msimu uliopita.
CONTE ANA HAKI YA KULALAMIKA
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment