Kama nilivyokuahidi kuwa nitakuletea majibu ya nyota wa Chelsea, Olivier Giroud kama ikitokea akitoa majibu ya sababu ya kumfata David Luiz wakati wa kushangilia goli alilolifunga kwenye mchezo uliopita wakati Chelsea ilipoifunga goli 1-0 klabu ya Liverpool na kufanikiwa kufikisha alama 69 kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza ambapo goli hilo lilifungwa na mfaransa huyo ambaye kwa sasa ana miaka 31.
Nyota huyo amefanyiwa mahojiano na kuulizwa kwanini aliamua kushangilia pamoja na mlinzi huyo ambaye kwa sasa anauguza majeraha yanayomfanya kuwa nje kwa muda mrefu.
"Niliamua kushangilia vile kwa kulielekeza goli lile kwa David Luiz maana ni rafiki yangu mkubwa na nahuzunishwa na kipindi kigumu anachokipitia" alisema mshambuliaji huyo raia waUfaransa.
Lakini pia kocha wa Chelsea, Antonio Conte aliulizwa juu ya ushangiliaji huyo alisema "Nadhani ni jambo la kawaida na uhusiano wao mkubwa naona kwa vile wote ni wachezaji wa timu moja"
No comments:
Post a Comment