Chelsea yatua tena kwa Edinson Cavani - Darajani 1905

Chelsea yatua tena kwa Edinson Cavani

Share This

Klabu ya Chelsea inatajwa kumfukuzia mshambuliaji wa klabu ya PSG, Edinson Cavani ili arithi pengo la Alvaro Morata ambaye anatajwa kufukuziwa na klabu ya Juventus.

Edinson Cavani ambaye ni raia wa Uruguay anatajwa kufukuziwa na Chelsea ili arithi nafasi ya Morata ambaye anatajwa kukamilisha makubaliano ya nyota huyo kujiunga na klabu ya Juventus ya nchini Italia, klabu ambayo aliwai kuichezea kabla ya kurejea Real Madrid na baadae kujiunga na Chelsea.

Cavani anatajwa kutokua kwenye mahusiano mazuri na nyota mwenzake wa PSG, Neymar ambaye tangu wajiunge pamoja kwenye klabu hiyo kumekua kukitaarifiwa kuwa na mgogoro kati yao na kama Chelsea ikionyesha nia nzuri ya kumtaka basi inaweza ikatumia kutokuelewana kwa nyota huyo ili kumnasa.

No comments:

Post a Comment