Chelsea kumtumia Willian ili kumnasa mchezaji wa Man utd - Darajani 1905

Chelsea kumtumia Willian ili kumnasa mchezaji wa Man utd

Share This

Huenda hii ikawa ni habari mbaya haswa kwa mashabiki wa Chelsea ambapo gazeti la Independent limechapisha habari kuwa winga wa Chelsea, Willian Borgea da Silva anakaribia kutua klabuni Manchester utd kwa mabadilishano na mchezaji Anthony Martial.

Chelsea imekuwa ikitajwa kumuwania winga Anthony Martial kutoka klabuni Manchester utd ambapo huko napo wametoa taarifa kua wanamuhitaji Willian kama sehemu ya usajili wa kumuachia Anthony Martial.

Martial aligoma kusaini mkataba mpya klabuni Manchester utd na tayari Chelsea na baadhi ya klabu nyengine barani Ulaya zimeshaonyesha nia ya kumtaka winga huyo raia wa Ufaransa.

Willian Borges da Silva amekua akihusishwa kutakiwa na klabu hiyo ya Manchester utd ingawa amewai kukaririwa kuwa hana mpango wa kuondoka klabuni Chelsea ingawa amekua na mahusiano mazuri na kocha wa Manchester utd, Jose Mourinho ambaye waliwai kufanya kazi pamoja pindi kocha huyo alipoifundisha klabu ya Chelsea.

No comments:

Post a Comment