Conte awazungumzia Bakayoko na Morata kwenye mkutano hii leo - Darajani 1905

Conte awazungumzia Bakayoko na Morata kwenye mkutano hii leo

Share This

Ilivyokawaida ni kwamba kila Chelsea inapoelekea kushuka uwanjani ili kucheza mchezo basi kocha Antonio Conte huwa na kawaida ya kufanya mkutano na waandishi wa habari kabla ya kuiongoza klabu yake kushuka uwanjani kucheza mchezo.

Mchana wa leo kocha huyo amefanya mkutano na waandishi hao wa habari ambapo siku ya kesho anategemea kuiongoza Chelsea kucheza mchezo wa ligi kuu Uingereza dhidi ya Huddersfield kwenye uwanja wa Stamford Bridge.

Na hapa nakuletea kwa ufupi baadhi ya mambo aliyoyaongelea kwenye mkutano huo alioufanya kwenye uwanja wa mazoezi wa Chelsea maarufu kama Cobham.

Aliulizwa juu ya mtazamo wake kuelekea kwenye mchezo wa kesho dhidi ya klabu hiyo ya Huddersfield ambapo kocha huyo alijibu kwa kusema anaiheshimu klabu hiyo ingawa anataka apate ushindi ili kujiweka sawa kwenye mbio zake za kugombania ubingwa.

Aliulizwa kuhusu majeraha ya mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata ambaye aliukosa mchezo uliopita dhidi ya Liverpool huku kocha huyo akisema majeraha yake si ya muda mrefu na anaweza akarejea haraka ambapo hilo pia ndilo lilikuwa jibu lake kwa leo hii akisema nyota huyo yupo ngangari kuiongoza Chelsea kwenye mchezo wa kesho.

Aliulizwa pia kuhusu kiwango cha nyota kiungo Tiemoue Bakayoko ambaye alikuwepo kwenye kikosi cha mchezo uliopita dhidi ya Liverpool ambapo kocha huyo alisema nyota huyo ni mchezaji bora anayecheza soka safi haswa katika mchezo dhidi ya Liverpool lakini pia akisema nyota huyo bado ana umri mdogo kwa maana hiyo bado ana muda mwingi wa kujiweka sawa.

Lakini pia kubwa ni lile swali aliloulizwa juu ya nafasi ya Chelsea kufudhu kucheza michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa msimu ujao ambapo kocha huyo alisema mpaka kufikia sasa haina haja ya kujutia kuhusu michezo iliyopita maana bado mapambano yanaendelea huku Chelsea ikiwa imebakiza michezo miwili ya ligi kuu (dhidi ya Huddersfield na Newcastle) lakini pia ikibakiza mchezo wa fainali ya kombe la FA dhidi ya Manchester utd.

No comments:

Post a Comment