Chelsea kucheza dhidi ya Liverpool usiku wa leo - Darajani 1905

Chelsea kucheza dhidi ya Liverpool usiku wa leo

Share This

Kikosi cha vijana cha Chelsea ambacho hiki kinajumuisha wachezaji kadhaa vijana katika akademi ya Chelsea ambacho chenyewe kinajiita Chelsea Development kinashuka uwanjani usiku huu wa leo kucheza mchezo wake wa ligi kuu Uingereza 2 maarufu kama Premier League 2 ambapo itacheza dhidi ya Liverpool.

Mchezo huo utakaochezwa kwenye uwanja wa Anfield ni muhimu kwa Chelsea iondoke na ushindi ambapo itafanikiwa kupanda katika nafasi tatu mpaka kufikia nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Callum Hudson-Odoi ni moja kati ya nyota watakaoshiriki kwenye mchezo huo dhidi ya Liverpool ambayo yenyewe inashika nafasi ya tatu na mchezo huo utachezwa saa 09:05 Usiku (Saa 21:05) kwa saa za Afrika Mashariki nami nitakuletea habari na matokeo kuhusu mchezo huo.

No comments:

Post a Comment