Tanzia, Chelsea yakumbwa na msiba mzito - Darajani 1905

Tanzia, Chelsea yakumbwa na msiba mzito

Share This

Katika jiji la London mchana wa leo kumeripotiwa kifo cha mchezaji wa zamani wa Chelsea lakini pia aliwai kuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo, Ray Wilkins ambaye amefariki kwenye hospitali ya St. George aliyokimbizwa wiki iliyopita mara baada ya kuugua mshtuko wa moyo.

Ray Wilkins aliyefariki akiwa na miaka 61 aliyewai kuwa mchezaji na nahodha wa Chelsea amepoteza maisha siku ya leo akiwa kwenye hospitali akiwa kwenye uangalizi maalum.

Mara baada ya taarifa hizo za huzuni, klabu ya Chelsea imetuma ujumbe mfupi kuonyesha huzuni zao juu ya taarifa hizo kwa kusema "Kila mtu mwenye mahusiano na klabu ya soka ya Chelsea amehuzunishwa na taarifa hii ya kifo cha gwiji wetu, nahodha wetu na kocha msaidizi wetu, Ray Wilkins. Pumzika kwa amani Ray, hakika kila mtu atakukumbuka"

Wakati wa taarifa za kuugua kwake kocha Antonio Conte, na wachezaji wa zamani wa Chelsea ambao waliwai kuwa chini yake alipokuwa kocha msaidizi wa kocha Carlo Ancellotti pindi alipoifundisha Chelsea, Didier Drogba na Frank Lampard nao walituma ujumbe kwa gwiji huyo.

Lakini nasi kama Darajani 1905 tunatuma salamu zetu za kuonyesha kuhuzunishwa na taarifa hizi...

No comments:

Post a Comment