Ancelloti atoa neno kifo cha gwiji wa Chelsea - Darajani 1905

Ancelloti atoa neno kifo cha gwiji wa Chelsea

Share This

Aliichezea Chelsea michezo 173 na kuifungia magoli 30, leo amepoteza maisha kwenye hospitali ya St. George huko nchini Uingereza kwenye jiji la London. Ni Ray Wilkins, mara baada ya kifo chake hicho kuna jumbe nyingi zimetolewa na watu tofautitofauti, lakini mmojawapo ni kocha muitaliano, Carlo Ancelloti ambaye walishawai kufanya kazi pamoja klabuni Chelsea huku Wilkins akiwa kama kocha msaidizi.

"Siku ya leo ni siku ya huzuni, tumempoteza mtu bora na rafiki mwema. Lilikuwa ni jambo la kuvutia kufanya kazi pamoja na Ray, pumzika kwa amani" alisema kocha huyo ambaye pindi wakiwa wanaifundisha Chelsea waliisaidia klabu hiyo kushinda taji la ligi kuu nchini Uingereza kwa msimu wa 2009-2010.

Lakini pia kupitia kitabu cha kocha huyo Carlo Ancelloti, kitabu cha The Beautiful Games of an Ordinary Genius, kocha huyo aliwai kuandika "Ray ni mmoja kati ya watu wachache, ambaye yupo sawa kwa kila jambo, mtu mwenye damu ya bluu [mapenzi ya Chelsa] Chelsea ilikuwa inatembea kwenye mishipa yake ya damu...bila ya yeye tusingeweza kushinda chochote"

Pumzika Kwa Amani Ray Wilkins

No comments:

Post a Comment