Bodi ya klabu ya Chelsea haionekani kuwa na mawasiliano mazuri na mahusiano mazuri na kocha wa klabu hiyo Antonio Conte kutokana na kocha huyo kuishutumu mara kadhaa juu ya mfumo wa usajili ulivyo klabuni hapo ambapo nafasi ya kocha katika usajili wa wachezaji iwe kwa kuuza au kununua ukiwa ni mdogo. Lakini pia Chelsea kuwa na msimu mbovu kwa sasa kunachochea jitihada za bodi ya klabu hiyo kutaka kuachana na kocha huyo. Na tayari inadhaniwa Chelsea itaachana na kocha huyo ifikapo mwishoni mwa msimu huu.
Kama kuondoka kwa kocha huyo raia wa Italia kukikamilika basi ni lazima nafasi yake ichukuliwe na kocha mwengine ambapo mpaka sasa wanatajwa makocha tofautitofauti, lakini kati ya makocha hao wanaotajwa kuna jina jipya limetajwa kwa mara ya kwanza kuwania nafasi ya kocha huyo.
Leonardo Jardim. Ni kocha wa klabu ya As Monaco na ndiye aliyesaidia klabu hiyo kuuvunja ufalme wa PSG ambao wamekuwa wakishinda mfululizo taji la ligi kuu huko nchini Ufaransa kabla ya mfululizo huo kuvunjwa msimu uliopita.
Kocha huyo anatajwa kuwa moja ya makocha waliofanyiwa mawasiliano na klabu ya Chelsea ili atue klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.
Makocha wengine wanaotajwa ni pamoja na Massimiliano Allegri [Juventus], Luis Enrique [Huru], Carlo Ancelloti [Huru]
No comments:
Post a Comment