Mchezaji na nahodha wa zamani wa Chelsea, Ray Wilkins amefariki mchana wa leo akiwa hospitali ya St. George ya nchini Uingereza kwenye jiji la London kutokana na matatizo ya moyo.
Mara baada ya kifo chake hicho, magwiji wengi na wapenda soka wengi wametoa jumbe zao za kuonyesha kuuzunishwa na taarifa hizo zilizokuja siku kadhaa mara baada ya kulazwa kwenye hospitali hiyo.
Lakini kati ya hao, ni gwiji mwenzake wa Chelsea, John Terry ambaye nae ametuma ujumbe kuhusiana na kifo cha nyota huyo wa zamani raia wa Uingereza aliyewai kuitumikia Chelsea kama mchezaji lakini pia kama kocha msaidizi.
Ujumbe huo ameutuma kupitia mtandao wa Instagram huku akieleza mambo mengi kama jinsi alivyosaidiwa kufikia mafanikio aliyoyafikia hapo alipo akimtaja mtu huyo kuwa alihusika kwa kiasi kikubwa akisema (John Terry) alipokuwa na miaka 17 alikuwa akiambiwa na gwiji huyo kuvaa viatu na kuingia uwanjani ili kufanya mazoezi lakini pia akielezea jinsi walivyocheza pamoja kipindi iko John Terry akiwa anachipukia kwenye soka la kiushindani.
Mambo mengi ameyaeleza lakini mwisho akaeleza juu ya hisia zake za huzuni kwa familia ya gwiji huyo aliyoiacha ambapo ameacha mke mmoja na watoto wawili.
No comments:
Post a Comment