Chelsea yatanguliza mguu mmoja fainali ya FA - Darajani 1905

Chelsea yatanguliza mguu mmoja fainali ya FA

Share This

Klabu ya vijana ya Chelsea ya chini ya miaka 18 imepata ushindi wake wa kwanza katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la FA kwa vijana mara baada ya kupata ushindi wa mabao 0-3 wakiwa ugenini dhidi ya klabu ya vijana ya Birmingham city.

Chelsea U18 iliyochini ya kocha Jody Morris ilipata magoli hayo matatu kupitia kwa Tariq Uwakwe aliyefunga goli dakika ya 15 huku Hudson-Odoi akiipatia Chelsea goli la pili mnamo dakika ya 33 na kufanya mchezo kwenda mapumziko huku Chelsea ikiwa mbele kwa magoli 0-2. Charlie Brown ndiye aliyekuwa mfungaji wa goli la tatu mara baada ya kuingia kama mchezaji wa akiba na kuifanya Chelsea iondoke na ushindi huo mnono katika mchezo wa kwanza huku mchezo wa marudiano ukitegemewa kufanyika wiki ijayo.

Lakini kabla ya kuanza kwa mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa St. Andrews, kulitanguliwa na kutolewa kwa heshima kwa mchezaji na kocha msaidizi wa zamani wa Chelsea, Ray Wilkins ambaye alikuzwa na kutokea kwenye kikosi cha vijana cha Chelsea ambaye amefariki dunia hapo jana kwenye hospitali ya St. George huko jijini London.

No comments:

Post a Comment