Wachezaji na makocha wa Chelsea kuhusu kifo cha Wilkins - Darajani 1905

Wachezaji na makocha wa Chelsea kuhusu kifo cha Wilkins

Share This
Jana kumeripotiwa taarifa za kifo cha mkongwe wa Chelsea aliyeitumikia klabu hiyo kama mchezaji kwa nafasi ya kiungo pamoja na kama kocha msaidizi, Ray Wilkins ambaye amepoteza maisha akiwa na miaka 61 huku akiacha watoto wawili na mke mmoja.

Mara baada ya kifo hicho, hapa nakuletea jumbe zilizotumwa na wachezaji wa zamani wa Chelsea pamoja na makocha kuhusu gwiji na nyota huyo raia wa Uingereza ambaye kwa sasa ni marehemu.

John Terry:
Huyu amemuelezea Wilkins kiupana haswa kutokana na muda mwingi waliotumia wakiwa pamoja klabuni Chelsea na hata baada ya gwiji huyo kuachana na Chelsea ambapo alijiunga na klabu ya Manchester united. Lakini kubwa ujumbe wake unahuzunisha pale alipojaribu kukumbushia mchango aliopata kutoka kwa gwiji huyo pindi alipokuwa na miaka 17. Na mwisho wa ujumbe wake alimalizia kwa kusema ataungana na familia ya gwiji huyo kwenye kila hali itakayotokea.

Didier Drogba;
Raia huyu wa Ivory Coast aliandika ujumbe mrefu pia huku akionyesha kuguswa yeye kama mchezaji aliyewai kuwa na msimu bora wa 2009-2010 huku gwiji huyo akiwa kocha msaidizi wa Chelsea ambapo katika msimu huo Didier Drogba alikuwa mfungaji bora wa ligi kuu lakini pia Chelsea ikitwaa mataji mawili ya ligi kuu Uingereza pamoja na kombe la FA ambapo Didier alisema msimu huo alipata mafanikio makubwa huku Wilkins akihusika kwa mafanikio yake kwa kiasi kikubwa.

Michael Ballack;
Huyu hakutuma ujumbe mrefu sana lakini kikubwa alionyesha kuhuzunishwa na taarifa za ghafla za kocha huyo kufariki dunia na akiamini alichangia mafanikio ya Chelsea kwa kiasi kikubwa.

Ashley Cole;
Aliandika ujumbe mrefu akikumbushia mengi aliyoyafanya na kushirikiana vyema na gwiji huyo huku akieleza mafanikio yake binafsi pamoja na ya klabu yalichangiwa kwa karibu na gwiji huyo.

Ruud Gullit;
Huyu aliwai kuwa kocha mchezaji wa klabu ya Chelsea ambapo alituma pia ujumbe wa kuonyesha kuhuzunishwa na taarifa hizo akituma ujumbe mfupi akieleza jinsi ya taarifa hizo zilivyo za huzuni.

Carlo Ancelloti;
Aliongea maneno machache ila yaliyoonyesha kwa kiasi gani anakiri na kuuthamini mchango wa gwiji huyo ambaye alikuwa msaidizi wake klabuni Chelsea akisema kufariki kwa gwiji huyo ni jambo la huzuni lakini pia akielezea ubora na tabia njema ya kocha huyo. Lakini pia kama hiyo haitoshi, kocha huyo muitaliano aliwai kuandika kitabu chake ambapo humo ndani alieleza umuhimu wa kocha huyo na kwa kiasi gani alichangia mafanikio ya Chelsea ilipokuwa chini yake.

Michael Essien;
Naye kupitia mtandao wa Instagram hakutuma ujumbe mrefu ila zaidi aliongelea kuhuzunishwa na taarifa za kifo cha kocha huyo.

Hao ni baadhi ya na wachezaji waliotumia mitandao mbalimbali ya kijamii kutuma jumbe za kuonyesha kwa kiasi gani msiba huo ulivyowashtusha.

No comments:

Post a Comment