Rasmi; Nyota wa Chelsea kutimkia Denmark - Darajani 1905

Rasmi; Nyota wa Chelsea kutimkia Denmark

Share This

Alisajiliwa na Chelsea toka mwaka 2010 lakini hajafanikiwa kuichezea klabu hiyo mchezo wowote mpaka sasa akiwa na miaka 25, ameishia kutolewa kwa mkopo tu huku akivichezea vilabu kumi kwa mkopo angali bado ni mchezaji wa Chelsea.

Anaitwa Matej Delac raia wa Croatia ambae aliwai kutamba na kikosi hicho cha timu ya taifa chini ya miaka 21. Lakini sasa muda wake wa kubaki kuwa mchezaji wa Chelsea umekwisha mara baada ya nyota huyo kusaini mkataba wa uhamisho huru wa kujiunga na klabu inayoshiriki ligi kuu nchini Denmark, klabu ya AC Horsens ambayo amesaini nayo mkataba mpaka mwaka 2020.

Delac alisajiliwa na Chelsea lakini katika kipindi chote hicho hajafanikiwa kuichezea Chelsea mchezo wowote kutokana na kukosa kibali cha kufanya kazi nchini Uingereza na hivyo sasa kukaribia kujiunga na klabu hiyo ambayo amekuwa akifanya nayo mazoezi ambayo imekubali kumsajili jumla kama mchezaji wa bure.

Mwezi Novemba aliwai kuhojiwa kama anajutia kujiunga na Chelsea akiwa na umri mdogo na kushindwa kuichezea mchezo wowote uliorasmi, nyota huyo alisema "Watu wengi wananifikiria hivyo kwamba najutia kutua Chelsea, lakini ukweli ni kwamba sijutii maana kucheza kwangu kwa mkopo kwenye klabu nyingi kumenifanya nikutane na makocha na wachezaji wengi walionifanya nipate uzoefu"

No comments:

Post a Comment