Wachezaji 8 wanaoweza kuondoka Chelsea - Darajani 1905

Wachezaji 8 wanaoweza kuondoka Chelsea

Share This
Chelsea imebakiza taji moja tu mkononi mwake ambalo inaweza ikalitwaa msimu huu, taji la kombe la FA. Lakini kushinda taji hilo hakutoifanya klabu hiyo ijisifu kwa kuwa na msimu mzuri.

Kushiriki kwake katika michuano minne na kubakiza taji moja, kunamaanisha Chelsea imekuwa na msimu mbaya ukijumlisha pia na nafasi yake finyu ya kufudhu kucheza michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa msimu unaokuja.

Kutokana na hali hiyo klabuni hapo, mtandao mmoja barani Ulaya umechapisha makala ya kuwaelezea wachezaji wa klabu hiyo wanaoweza kuachana na klabu hiyo ifikapo mwishoni mwa msimu.

Thibaut Courtois
Familia yake kuishi nchini Hispania kunatajwa kumfanya mlinda mlango huyo kuonekana hana maisha marefu klabuni hapo haswa pia ukizingatia kukataa kwake kusaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki Chelsea kunaweza kuifanya klabu hiyo kulazimika kumuuza na kutimkia Real Madrid.

Cesc Fabregas
Anaonekana kuzidiwa sana na kasi ya mchezo kwa sasa, haswa kutokana na umri wake kuelekea kumtupa mkono. Lakini pia ujio wa Ross Barkley kunamfanya mhispania huyo mwenye miaka 30 kuwa na nafasi finyu ya kubaki klabuni Chelsea haswa kutokana na kubakiza mkataba wa mwaka mmoja kunaweza kuifanya Chelsea kumweka sokoni ili kupata fungu kabla hajaondoka bure pale mkataba wake utakapoisha.

Gary Cahill
Ameanza kwenye michezo 21 kati ya 31 msimu huu, huku akiachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kilichocheza michezo yake ya kirafiki kunaweza kumfanya mkongwe huyu kuachana na Chelsea haswa kutokana na nafasi yake kuonekana anatumika sana Antonio Rudiger.

Eden Hazard
Mpaka sasa anatajwa kuwa chaguo la kwanza la kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane, lakini pia amekuwa akihusishwa kutakiwa na klabu hiyo ya nchini Hispania huku mwenyewe akikataa kusaini mkataba mpya klabuni Chelsea. Lakini pia kutokana na nukuu ya baba yake mzee Thierry Hazard kwamba nyota huyo amekataa kusaini Chelsea ili ajiunge na Real Madrid kunazidi kuchochea na huenda ikakamilika pale tu Chelsea itakaposhindwa kucheza klabu bingwa barani Ulaya msimu ujao.

Olivier Giroud
Alitua Chelsea akitokea Arsenal kwa dau la paundi milioni 18 huku akisaini mkataba wa miezi 18 ambapo hiyo inamaanisha mpaka kufikia tarehe 30-Juni itamaanisha mshambuliaji huyo raia wa Ufaransa atakuwa amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake klabuni Chelsea, lakini inaaminika kutokana na umri wake wa miaka 31, alisajiliwa na Chelsea ili kuisaidia klabu hiyo kutetea mbio zake za kushinda mataji msimu huu na mara baada ya msimu kuisha kutaaminisha kuondoka kwa nyota huyo.

Pedro Rodriguez
Amebakiza mwaka mmoja tu kwenye mkataba wake wa kuwa mchezaji wa Chelsea, umri wake wa miaka 30 kunaifanya Chelsea ianze kusaka nyota mwengine mwenyr umri mdogo na hivyo kutakiwa kwa nyota wa Bayer Leverkusen, Leon Bailey kunaweza kufungua milango kwa mhispania huyu kuondoka Chelsea.

Kurt Zouma
Kabla ya kujiunga kwa mkopo na klabu ya Stoke city, Kurt Zouma alisaini mkataba mpya wa kuendelea kuwa mchezaji wa Chelsea. Amekuwa na msimu mzuri klabuni Stoke city licha ya kuwepo kwenye nafasi mbaya ya msimamo wa ligi kuu Uingereza lakini kucheza kwake michezo 28 kutamfanya nyota huyo raia wa Ufaransa kuhitaji nafasi kwenye kikosi cha  Chelsea pindi atakaporejea.

Michy Batshuayi
Aliondoka Chelsea mwezi Januari katika dirisha dogo la usajili  na kujiunga na Borrusia Dortmund kwa mkopo, amekuwa na msimu mzuri toka ajiunge na klabu hiyo akihusika vyema kwenye ufungaji. Lakini mafanikio hayo yanamaanisha kutaka kutumika kama mshambuliaji chaguo la kwanza endapo atarejea Chelsea ambapo hiyo haitokuwa rahisi. Rais wa klabu hiyo ya Dortmund aliwai kukiri alitaka kumsajili mbelgiji kuonyesha kuwa wana uhitaji nae ambapo hiyo inatafsiriwa kama kusalia kwa nyota klabuni hapo.

No comments:

Post a Comment