Abramovich kumalizana na Conte - Darajani 1905

Abramovich kumalizana na Conte

Share This

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte haonekani kuendelea kuwa kocha wa Chelsea mara baada ya msimu huu kuisha, kutokana na hali na mwenendo wa Chelsea ulivyo kwa sasa haswa ikitegemea klabu hiyo kuwa na nafasi finyu ya kufudhu kucheza michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa msimu ujao.

Kuna makocha kadhaa waliwai kupita klabuni hapo na wamekuwa hawana mwisho mzuri mara baada ya kushindwa kufanya vizuri kwenye michuano ya klabu bingwa mmojawapo alikuwa kocha Andre Villas Boas, ambapo hiyo inaifanya nafasi ya kocha Antonio Conte kuwa na nafasi finyu ya kuendelea kusalia klabuni hapo haswa akishindwa kufudhu kucheza michuano hiyo.

Mmiliki wa klabu hiyo, Roman Abramovich anatajwa kuwa tayari kutoa donge nono ili kumalizana na kocha huyo kama malipo ya mkataba uliosalia kwenye mkataba aliosaini kocha huyo alipoisaidia kushinda taji la ligi kuu Uingereza.

Dau la paundi milioni 9.5 linatajwa kuhusika kama mmiliki Abramovich ataamua kumtimua kocha huyo ambapo ni dau linalotajwa kumlipa kocha huyo kama malipo ya mwaka mmoja ambao amebakiza kwenye mkataba wake.

No comments:

Post a Comment