Kocha wa klabu ya Juventus ya nchini Italia, Massimiliano Allegri ameeleza mipango yake ya baadae kama akiachana na klabu hiyo ya Turin ya nchini humo. Kocha huyo anadai kama akiondoka ama kuachana na klabu hiyo basi anatazamia kujiunga na klabu iliyonje ya nchi ya Italia.
Kocha huyo ambaye alitua klabuni hapo kuchukua nafasi ya kocha wa sasa wa Chelsea, Antonio Conte ambaye kwa kipindi iko aliungana na timu ya taifa ya Italia kabla ya kutua Chelsea anasema kuachana kwake na klabu ya Juventus basi kutamaanisha kujiunga kwake na klabu tofauti kabisa iliyonchini Italia na hivyo kuzishtua klabu kadhaa barani Ulaya ambazo zimekuwa zikitajwa kuhitaji huduma ya kocha huyo mwenye miaka 50 sasa.
Chelsea nayo ni klabu mojawapo inayotajwa kumhitaji kocha huyo muitaliano kama ikiachana na kocha wake wa sasa, Antonio Conte ambaye haonekani kuwa na muda mrefu wa kuendelea kuwa kocha wa klabu hiyo aliyoshinda nayo taji la ligi kuu Uingereza katika msimu wake wa kwanza wa 2016-2017.
No comments:
Post a Comment