Hii ni wiki mbaya kwa klabu na mashabiki wa Chelsea mara baada ya hapo jana kupoteza mchezo wake muhimu wa ligi kuu Uingereza ikiwa nyumbani dhidi ya Tottenham. Mchezo ambao kwa Chelsea ilitakiwa ipate ushindi kwa aina yoyote ili ajiweke sawa katika kugombania nafasi nne za juu ambazo kisheria zitafudhu kucheza michuano ya klabu bingwa Ulaya msimu ujao.
Mara baada ya kupoteza mchezo huo dhidi ya klabu hiyo ya jijini London, nahodha msaidizi wa Chelsea, Cesar Azpilicueta ametoa neno juu ya nini kilisababisha Chelsea ipoteze mchezo huo.
"Kiukweli tulistahili kuondoka na ushindi, haswa katika kipindi cha kwanza ambapo tulitengeneza nafasi nyingi, lakini tatizo lilianzia tuliporuhusu kufungwa goli moja, goli ambalo lilimaanisha kutoka sare kwa kipindi hiko cha kwanza" alisema nahodha huyo msaidizi ambaye ni raia wa Hispania.
Chelsea ilifanikiwa kupata goli la kwanza na kuongoza mchezo huo, goli lililofungwa na Alvaro Morata kabla ya mchezaji wa Tottenham, Christian Eriksen kuchomoa goli hilo katika dakika za majeruhi za kipindi cha kwanza na kufanya kipindi hiko kuisha kwa sare ya 1-1. Kipindi cha pili Chelsea ilionekana kuzidiwa sana na hivyo Delle Alli kuifungia klabu yake magoli mawili yaliyoifanya timu hiyo kupata ushindi wake wa kwanza dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Stamford Bridge kwa miaka 28.
No comments:
Post a Comment