PSG waifata Chelsea kwa ushawishi mwengine - Darajani 1905

PSG waifata Chelsea kwa ushawishi mwengine

Share This

Nyota wa klabu ya Chelsea, N'Golo Kante amebakiza mkataba wa miaka mitatu wa kuitumikia klabu ya Chelsea lakini pia ndiye chaguo la kwanza kwenye usajili kwa klabu ya PSG ambayo inamtaka kiungo huyo ili itimize adhma yake ya kushinda taji la klabu bingwa barani Ulaya (Uefa Champions League).

Kuonyesha kwamba klabu hiyo inamtaka Kante kuna taarifa zinadai kwamba klabu hiyo inakubali kumruhusu kiungo wake, Adrien Rabiot ajiunge na Chelsea kama sehemu ya mabadiliko ya kumpata Kante mwenye miaka 27.

Taarifa zilizopo zinadai kwamba Chelsea inahitaji paundi milioni 88 ili kumuuza Kante kwenda kwa klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Ufaransa wakati PSG wao wanataka kumtumia Rabiot mwenye miaka 23 ambaye amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake huku akiwa na thamani ya paundi milioni 44 kama sehemu ya mabadiliko ya kumpata Kante.

Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment