Chelsea inatajwa kupambana dhidi ya Manchester city katika kugombania saini ya kiungo raia wa Italia, Jorginho anayeichezea klabu ya Napoli ya nchini kwao Italia.
Mwanzoni Manchester city ilikuwa ikipewa nafasi kubwa ya kumnasa kiungo huyo lakini sasa Chelsea imepewa nguvu kubwa ya kumnasa kiungo huyo mwenye asili ya Brazil.
Kupitia mtandao wa Instagram, mke wa nyota huyo alituma ujumbe wa picha ukimuonyesha yupo kwenye ndege akisafiri ingawa haikujulikana wapi anaelekea ingawa inadhaniwa anasafiri ili kuongozana na mme wake kutua Uingereza ili kukamilisha usajili. Lakini sababu inayoelezwa kuipa nguvu Chelsea kumnasa nyota huyo ni kutokana na mama mzazi wa nyota huyo kuifatilia (follow) akaunti ya Chelsea kwenye mtandao wa Instagram.
Taarifa zinaeleza mama huyo kuifatilia akaunti ya Chelsea kunaipa nguvu Chelsea katika jitihada zake za kumnasa nyota huyo.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment