Hatimaye Mungu ametuneemesha kuifikia ile siku kila mpenda michezo haswa mpenda soka alikuwa anatamani aifikie bahati mbaya kwa wale waliotangulia mbele za haki au kuwa mahututi mahospitalini lakini kubwa kila jambo linatokea kwa sababu maalumu na Mungu wetu hakoseagi pale anaporuhusu jambo fulani litokee.
Ni siku ya nusu fainali, ni siku ya vita ya timu mbili kubwa barani Ulaya lakini pia ni siku ya vita ya nyota wa Chelsea watakaoziongoza timu zao kucheza mchezo mmoja mkali wa nusu fainali utakaoamua nani wa kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Dunia.
Ufaransa ambayo ndiyo timu pekee kuwai kushinda Kombe la Dunia mpaka kufikia sasa itakuwa uwanjani kumenyana dhidi ya timu yenye kizazi cha dhahabu kwa sasa, Ubelgiji.
Ni vita ya Kante dhidi ya Hazard, Olivier Giroud dhidi ya Thibaut Courtois huku Michy Batshuayi akiwa yupo tayari kuongeza nguvu pale Ubelgiji itakapohitaji uwepo wake uwanjani.
Je nani ataibuka kuwa bingwa kwenye mchezo huu? nami naamini timu itakayoondoka na ushindi jioni ya leo ndiyo itakuwa na uwezekano mkubwa wa kumtoa mchezaji bora wa mashindano haya.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment