Kenedy akaribia kutua Newcastle - Darajani 1905

Kenedy akaribia kutua Newcastle

Share This

Winga na mlinzi wa kushoto wa Chelsea, Kenedy Robert anakaribia kujiunga kwa mkopo kwenye klabu ya Uingereza inayoshiriki ligi kuu nchini humo, klabu ya Newcastle united.

Kenedy anatajwa kubakiza vipimo ili aungane na klabu hiyo ambayo kwa sasa inajiandaa kucheza michezo yake ya kirafiki kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya.

Nyota huyo raia wa Brazil alitumia nusu msimu uliomalizika akiwa kwa mkopo kwenye klabu hiyo inayofundishwa na kocha wa zamani wa Chelsea, Rafa Benitez. Jambo la kushangaza kwenye mkataba wake wa mkopo kwenye klabu hiyo kuna kipengele cha kuuzwa kabisa mara baada ya mkopo kumalizika mara baada ya msimu mmoja.

Kipengele hicho kinamaanisha Newcastle itakuwa na uwezo wa kumsajili jumla nyota huyo endapo wakipendezwa na muda wake wa mkopo klabuni hapo.

Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment