Mara baada ya Chelsea kusafiri mpaka St. Mary's park kucheza mchezo wake wa nane dhidi ya Southampton, ligi kuu itakwenda mapumziko wiki moja ili kupisha michezo mingine ya kimashindano kisha wiki inayofata itarudi tena ambapo safari hiyo Chelsea itakuwa nyumbani kwake ikicheza dhidi ya wapinzani wao Manchester united.
Mchezo huu utavuta hisia na macho ya wengi haswa kutokana na ukubwa wa klabu hizo, Chelsea ikiwa imekuja kuvunja falme zilizojengwa na timu kongwe wakati Manchester united ikijivunia utajiri wake wa historia kwa kujiwekeza mapema na kufikia rekodi nyingi lakini ubabe wa Chelsea ulioanza rasmi kutokana na mapinduzi aliyoyafanya tajiri wa kirusi, Roman Abramovich toka alipoinunua klabu hiyo mwaka 2003 umeifanya Chelsea kubeba mataji mengi kuliko klabu yoyote pale Uingereza. Ikiwa imebeba mataji 15 wakati Manchester united wakibeba mataji 14.
Lakini pia kuelekea kwenye mchezo huu, Chelsea ina rekodi nzuri dhidi ya Manchester united ambapo toka kocha Antonio Conte aanze kuifundisha Chelsea, ameshuhudia timu yake ikipoteza michezo miwili tu kati ya michezo 6, tena michezo hiyo miwili akipoteza wakati Chelsea ikiwa ugenini kwa Man utd lakini Chelsea imepata ushindi kwenye michezo 4 kati ya hiyo 6, mitatu ikiwa nyumbani Stamford Bridge lakini mwengine ukiwa pale kwenye uwanja wa taifa wa Uingereza, Wembley Stadium katika fainali ya Kombe la FA mwezi May mwaka huu.
Lakini pia ukiangalia kwa rekodi za Stamford Bridge, mara ya mwisho kwa Chelsea kupoteza kwenye uwanja huo ilikuwa mwaka 2012 wakati Chelsea ilipopewa kadi nyekundu mbili na kupoteza kwa magoli 2-3.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment