Hatimaye timu ya taifa ya Ubelgiji inatupwa nje kwenye michuano ya Kombe la Dunia kwenye hatua ya nusu fainali mara baada ya kufungwa goli 1-0 dhidi ya Ufaransa na hii inamaanisha Ubelgiji itacheza mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu siku moja kabla ya mchezo wa fainali kuchezwa.
Ubelgiji inaisubiri timu itakayofungwa kati ya Uingereza dhidi ya Croatia utakaochezwa kesho tarehe 11-Julai.
Lakini pia ushindi huo wa Ufaransa unamaanisha timu hiyo imefanikiwa kufika fainali ya michuano hiyo ya Kombe la Dunia ambapo itamsubiri mshindi katika mchezo kati ya Uingereza dhidi ya Croatia.
Hii inamaanisha nini kwa Chelsea? hii inamaanisha Chelsea imefanikiwa kutoa nyota wawili watakaocheza fainali ya michuano hiyo inayoendelea huko nchini Urusi. N'Golo Kante na Olivier Giroud wanafanikiwa kufika hatua hiyo ya fainali ikiwa ni mara ya kwanza kwao kufika hatua hiyo.
Hongera kwao, lakini pole kwa Eden Hazard, Thibaut Courtois na Michy Batshuayi ambao wameshindwa kufudhu kucheza fainali.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

Kombe la Dunia; Kante, Giroud watangulia fainali
Share This
Tags
# Chelsea FC
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea FC,
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment