Nusu fainali ya kwanza kwenye michuano ya Kombe la Dunia itachezwa tarehe 10-Julai kati ya Ufaransa dhidi ya Ubelgiji.
Mchezo huu unakutanisha nyota watano kutoka klabu ya Chelsea ambapo kwa upande wa Ufaransa kuna nyota wawili ambao ni Olivier Giroud pamoja na N'Golo Kante wakati kwa Ubelgiji kuna nyota watatu ambao ni Eden Hazard, Michy Batshuayi na Thibaut Courtois.
Kuelekea kwenye nusu fainali hiyo, mshambuliaji Olivier Giroud ameulizwa kuhusu nani bora kati ya mlinda mlango Hugo Lloris ambaye ni mlinda mlango wa Ufaransa na kipa Thibaut Courtois ambaye wanacheza klabu moja ya Chelsea.
Nyota huyo alijibu kwa kumsifia Courtois kwa kusema ni kipa mzuri mwenye uwezo wa kuokoa mashambulizi katika sehemu yoyote akiwa golini na huwa anapata ugumu sana kumfunga pindi wanapokuwa mazoezini na anaamini makipa hao wote wanastahili kushinda tunzo ya kipa bora wa michuano ya Kombe la Dunia kwa mwaka 2018 lakini mwisho akaja kusema Lloris ambaye ni kipa wa klabu ya Tottenham ni bora kuliko Thibaut.
Je ni kweli?
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment