Ni Chelsea dhidi ya Liverpool kwenye mchezo wa saba wa ligi kuu Uingereza msimu wa 2018-2019, mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge, mchezo utakaochezwa siku saba toka Chelsea kucheza mchezo wa watani wa jadi kutoka jiji la London (London derby) dhidi ya West Ham. Tuingie kwenye uchambuzi.
Mchezo huu utakuja huku Liverpool wakitaka kulipiza kisasi kutokana na mchezo uliopita katika uwanja huu kupigwa 1-0 shukrani kwa goli pekee lililofungwa na Olivier Giroud akitumia krosi nzuri iliyopigwa na Victor Moses. Lakini pia watataka kulipiza kisasi kutokana na kushindwa kupata ushindi dhidi ya Chelsea kwa msimu uliopita ambapo kama una kumbukumbu vyema mchezo wa kwanza tuliocheza kwao pale Anfield uliisha kwa sare ya 1-1 goli lao likifungwa na Mohammed Salah ambaye ushangiliaji wake ulitafsiriwa kama kuwaomba radhi Chelsea lakini tena huku Willian akaingia kama mchezaji aliyetokea benchi na kufunga goli tamu kabisa ambalo mwisho wa siku alihojiwa akiulizwa kama hakuwa na lengo la kufunga ila kupiga krosi ila mwenyewe alijibu akisema alilenga kufunga.
Turudi kwenye uchambuzi. Mchezo huu wa tarehe 29-Septemba utakuwa muhimu sana kwa Chelsea kuhakikisha tunapata ushindi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya msimamo wa ligi kuu. Ni vyema kuhakikisha tunaondoka na ushindi katika michezo yote ambayo tutakuwa nyumbani tukicheza dhidi ya timu sita za juu ili ata kama tukienda kwao tukipata sare michezo yote basi tutakuwa na alama 24 ambazo ni sawa na ushindi kwenye michezo nane. Hii inakuweka kwenye nafasi nzuri ya kupambania ubingwa.
Miaka miwili toka kuanzishwa kwa Chelsea, ilikutana kwa mara ya kwanza na majogoo hao wa jiji mwaka 1907 katika mchezo wa ligi daraja la kwanza (kwa sasa ni ligi kuu Uingereza) na kushuhudiwa Chelsea ikiondoka na ushindi wa mabao 1-4 ikiwa ugenini wakati kwenye michezo mitano ya mwisho kwa klabu hizo kushinda, Chelsea imeshinda mmoja huku ikipoteza mmoja na kutoa sare michezo mitatu.
Kiujumla toka kukutana mara ya kwanza kwa klabu hizo, Liverpool imepata ushindi kwenye michezo 77 huku Chelsea ikipata ushindi kwenye michezo 62 na kutoa sare michezo 40!
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment